Siku ya Alhamis
tarehe 18.2.2016 ni moja ya siku iliyokuwa ya kihistoria nchini
Uganda,nahiita siku hiyo ya kistoria kwa sababu ya uchaguzi mkuu uliofanyika
nchini humo siku hiyo.Ulikuwa ni uchaguzi wa kihistoria kwa sababu mbalimbali;
mosi, ni uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na wagombea urais yaani
wagombea watatu kukubalika mno na kuwa
na ushawishi mkubwa kwa wananchi,na wagombea hao ni Yoweri Kaguta Museveni wa chama cha NRM,Dk Kiiza Besigye wa FDC na
Amama Mbabazi.Pili ni uchaguzi uliotanguliwa na mdahalo wa wagombea urais
kipindi cha kampeini ambapo kila mmoja
wao alijieleza nini angefanya kama angepewa ridhaa na wananchi
Ni dhahiri watu wengi walikuwa na shauku ya kutakakjua
na kuona jinsi zoezi zima la uchaguzi litakavyoenda,hiyo inaweza kudhihirishwa
na vyombo vya habari kutoka ndani na nje jinsi vlivyomulika zoezi zima la uchaguzi na pia mitandao ya kijamii nayo haikuwa nyuma
kuhakikisha watu wanapashana habari
katika zoezi hilo
Naweza kusema ni uchaguzi uliogubikwa na matukio
mengi mpaka kutiliwa shaka kwa jinsi zoezi lilivyoendeshwa na mambo mbalimbali
yaliyojitokeza kipindi cha uchaguzi huo.Moja ya matukio hayo,ni jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa pasipo
sababu ya msingi kwa kuwakamata wananchi na viongozi wa upinzani.Kwa mfano kuna
baadhi ya wananchi na viongozi wa
upinzani kama Dk Kiiza Besigye kukamatwa na jeshi la polisi zaidi ya mara mbili
na ofisi ya Chama Chake Cha FDC kuvamiwa pasipo sababu za msingi.Tatu ni nyumba
za viongozi wa upinzani kama Amama Mbabazi kuzingirwa na jeshi la polisi
nyakati tofauti
Hayo ni matukio makubwa yaliyojitokeza katika
kipindi hicho cha uchaguzi.Hata hivyo, kuna kasoro mbalimbali zilizojitokeza
kipindi hicho,na kasoro hizo ni vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema
lakini vifaa vya kupigia kura kutokifa vituoni mapema na kuletwa dakika za
mwisho muda wa kupiga kura ukiwa unakaribia kuisha na matokeo ya uchaguzi
vituoni kuzidi idadi halisi ya wananchi waliojiandikisha katika vituo hivyo.Kwa
hiyo matukio hayo na kasoro hizo zinabaki kuibua maswali mengi kwa watu wengi.
Maswali hayo yanayoibuka ndani ya vichwa vya watu
wengi ni kwanini jeshi la polisi lilitumia
nguvu kubwa kukamata wananchi na
viongozi wa upinzani na kuvamia ofisi za vyama vyao pasipo sababu za msingi na walifanya hivyo kwa
malengo yapi na kutumwa na nani?. Na inakuaje kasoro nyingi, mfano namba ya
wapiga kura kuzidi namba halisi ya watu waliojiandikisha katika vituo hivyo?Je
chombo husika yaani tume hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na aina ya
udanganyifu wowote, au tume iliamua kufumbia macho kasoro hizo kwa kuweza
kukibeba chama kilichokuwa madarakani?
Kama Afrika tumeamua kukubali mfumo wa vyama vingi
basi tuwe tayari kukabiliana na matokeo ya mfumo huo,ni dhahiri na imezoeleka
kuwa vyama vinavyokuwa madarakani pale
uchaguzi unapokaribia kufanyika matukio mengi yamekuwa yakijitokeza,yaani
serikali iliyopo madarakani kutumia kila njia kutaka kushinda uchaguzi kwa
kukiuka taratibu na kujenga taswira machoni mwa watu kwa vyama vya upinzani kuonekana kama
chanzo cha vurugu katika chaguzi.
Nafikiri
ifike pahala watawala watambue kuwa vyama vya upinzani vinaweza kuongoza
nchi kama wananchi wameamua kuvipa ridhaa,hivyo maamuzi hayo yaheshimiwe kwa
sababu wananchi ndiyo wenye nchi na ni jukumu lao kuamua nani atakuwa kiongozi
wao, isitumike nguvu kubwa ya chama tawala kutumia nguvu dora kuhakikisha uamzi
wa watu unaingiliwa.Tumeamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi,hivyo tuwe tayari
kukubali matokeo ya mfumo huo.
Chagulani,Shabiru
25.2.2016