2/12/2015

Tuna kila sababu ya kupiga kura ya HAPANA dhidi ya katiba pendekezwa

Muda mfupi kuanzia sasa kutakuwepo upigaji wa kura ya maoni ili kuweza kuipitisha katiba iliyopendekezwa na bunge maalum la katiba.
Rai yangu kwa wananchi,tuna kila sababu ya kupiga kura ya hapana dhidi ya katiba iliyopendekezwa.Kwanza kuna mambo mengi yaliyokiukwa na pengine kwa maksudi kabisa ili kuweza kulinda maslahi ya wachache,kazi ya bunge maalum la katiba baada ya timu ya jaji Warioba kutimiza wajibu wao na kukabidhi rasimu hiyo kwa mh Rais,bunge  maalum kazi yake ilikua ni kujadili maoni hayo na kuyaboesha pale itakapohitajika.

Lakini bunge maalum halikuweza kufanya hivyo na baadala yake baadhi ya vifungu kutolewa na baadhi yake kubadilishwa kabisa,mfano mwananchi alikuwa na uwezo wa kumwajibisha mwakilishi wake (Mbunge) pale ambapo mwakilishi hakuweza kutimiza wajibu wake na kile ambacho aliahidi kwa wananchi,pili ubunge ulikuwa na ukomo ili kuweza kuwapa wananchi wengine fursa baada ya mbunge kutimiza muda kadhaa bungeni.
Hayo yote yalikuwemo katika rasimu ila ilipopelekwa bungeni yaliweza kuondolewa kabisa na mwananchi kunyimwa mamlaka hayo.

Hii ilifanyika maksudi kabisa ili kuweza kulinda maslahi ya wachache pale watakapokuwa madarakani hata kama mambo yasipoenda sawa yaani hata kama wasipotimiza wajibu wao hakuna wa kuwawajibisha..
Hivyo ukiukwaji huo ni dhahiri kuwa mawazo yetu sisi kama wananchi yameondolewa  na kuwapa fursa watawala kufanya wanavyotaka ilimradi wana kinga ya kikatiba..
Sasa kwa hali hii tunayo kila sababu ya kupiga kura ya hapana ili katiba pendekezwa wenye kulinda maslahi ya watu wachache yaani watawala haipiti.


Chagulani Shabiru