2/25/2016

Uganda na Ulaghai katika Demokrasia

Siku ya Alhamis  tarehe 18.2.2016 ni moja ya siku iliyokuwa ya kihistoria nchini Uganda,nahiita siku hiyo ya kistoria kwa sababu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo siku hiyo.Ulikuwa ni uchaguzi wa kihistoria kwa sababu mbalimbali; mosi, ni uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na wagombea urais yaani wagombea watatu kukubalika mno  na kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi,na wagombea hao ni Yoweri Kaguta Museveni  wa chama cha NRM,Dk Kiiza Besigye wa FDC na Amama Mbabazi.Pili ni uchaguzi uliotanguliwa na mdahalo wa wagombea urais kipindi cha kampeini  ambapo kila mmoja wao alijieleza nini angefanya kama angepewa ridhaa na wananchi
Ni dhahiri watu wengi walikuwa na shauku ya kutakakjua na kuona jinsi zoezi zima la uchaguzi litakavyoenda,hiyo inaweza kudhihirishwa na vyombo vya habari kutoka ndani na nje jinsi vlivyomulika zoezi zima la uchaguzi  na pia mitandao ya kijamii nayo haikuwa nyuma kuhakikisha watu wanapashana habari  katika zoezi hilo
Naweza kusema ni uchaguzi uliogubikwa na matukio mengi mpaka kutiliwa shaka kwa jinsi zoezi lilivyoendeshwa na mambo mbalimbali yaliyojitokeza kipindi cha uchaguzi huo.Moja ya matukio hayo,ni  jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa pasipo sababu ya msingi kwa kuwakamata wananchi na viongozi wa upinzani.Kwa mfano kuna baadhi ya wananchi  na viongozi wa upinzani kama Dk Kiiza Besigye kukamatwa na jeshi la polisi zaidi ya mara mbili na ofisi ya Chama Chake Cha FDC kuvamiwa pasipo sababu za msingi.Tatu ni nyumba za viongozi wa upinzani kama Amama Mbabazi kuzingirwa na jeshi la polisi nyakati tofauti
Hayo ni matukio makubwa yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha uchaguzi.Hata hivyo, kuna kasoro mbalimbali zilizojitokeza kipindi hicho,na kasoro hizo ni vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema lakini vifaa vya kupigia kura kutokifa vituoni mapema na kuletwa dakika za mwisho muda wa kupiga kura ukiwa unakaribia kuisha na matokeo ya uchaguzi vituoni kuzidi idadi halisi ya wananchi waliojiandikisha katika vituo hivyo.Kwa hiyo matukio hayo na kasoro hizo zinabaki kuibua maswali mengi kwa watu wengi.
Maswali hayo yanayoibuka ndani ya vichwa vya watu wengi ni kwanini  jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa  kukamata wananchi na viongozi wa upinzani na kuvamia ofisi za vyama vyao  pasipo sababu za msingi na walifanya hivyo kwa malengo yapi na kutumwa na nani?. Na inakuaje kasoro nyingi, mfano namba ya wapiga kura kuzidi namba halisi ya watu waliojiandikisha katika vituo hivyo?Je chombo husika yaani tume hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na aina ya udanganyifu wowote, au tume iliamua kufumbia macho kasoro hizo kwa kuweza kukibeba chama kilichokuwa madarakani?
Kama Afrika tumeamua kukubali mfumo wa vyama vingi basi tuwe tayari kukabiliana na matokeo ya mfumo huo,ni dhahiri na imezoeleka kuwa vyama vinavyokuwa madarakani  pale uchaguzi unapokaribia kufanyika matukio mengi yamekuwa yakijitokeza,yaani serikali iliyopo madarakani kutumia kila njia kutaka kushinda uchaguzi kwa kukiuka taratibu na kujenga taswira machoni  mwa watu kwa  vyama vya upinzani  kuonekana kama  chanzo cha vurugu katika chaguzi.
Nafikiri  ifike pahala watawala watambue kuwa vyama vya upinzani vinaweza kuongoza nchi kama wananchi wameamua kuvipa ridhaa,hivyo maamuzi hayo yaheshimiwe kwa sababu wananchi ndiyo wenye nchi na ni jukumu lao kuamua nani atakuwa kiongozi wao, isitumike nguvu kubwa ya chama tawala kutumia nguvu dora kuhakikisha uamzi wa watu unaingiliwa.Tumeamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi,hivyo tuwe tayari kukubali matokeo ya mfumo huo.
Chagulani,Shabiru

25.2.2016

2/10/2016

Mazungumzo ni bora kuliko uchaguzi kurudiwa Zanzibar

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa kihistoria katika jamhuri ya muungano wa Tanzania, yaani kwa kuwa na matukio makubwa, tukio la kwanza ni uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.Nauhita mwaka wa kihistoria kutokana na kampeni za uchaguzi pamoja na uchaguzi wenye kuwa na tofauti na miaka mingine iliyopita toka nchi ipate uhuru.Utofauti huo ni ushindani mkubwa uliokuwepo kwa vyama vya siasa na jinsi kampeni zilivyoendeshwa.Uchaguzi kwa Tanzania bara naweza kusema ulifanyika vizuri pamoja na kasoro za hapa na pale kujitokeza lakini kwa Tanzania visiwani yaani Zanzibar zoezi la uchaguzi halikumalizika vizuri kwa  maana ya matokeo ya uchaguzi kufutwa.
Uchaguzi huo ulifutwa kwa kile kinachodaiwa kuwa uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi ambazo zilipelekea chombo chenye mamalaka yaani tume ya uchaguzi Zanzibar( ZEC) kupitia mwenyekiti wake kutangaza kufutwa kwa uchaguzi kwa sababu kuu niliyoileza hapo awali.Hali hiyo imepelekea kile kinachoitwa mkwamo wa kisiasa( Political impasse).Mkwamo huo wa kisiasa umeibua maswali mengi kwa watu mbalimbali na taasisi mbali mbali,kwa mujibu wa waangalizi wa ndani na nje wanasema zoezi lilienda vizuri hakuna kasoro zilizojitokeza kama inavyodaiwa na tume,wapo wengine wanauliza uhalali wa tume kwa maana ya tume kuwa zinajitokezaje kasoro kubwa zinazopelekea mpaka matokeo yote ya ya uchaguzi kufutwa, je tume haikuwa imejiandaa kuhakikisha zoezi linafanyika kwa weredi? Na wengine wanadai kitendo cha mwenyekiti kufuta matokeo bila kamati kukaa ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria ilivyo/inavoelekeza.
Hatuwezi kupuuza wasiwasi wa watu hao walionao juu ya kilichotokea Zanzibar.Kama  wakaguzi wa ndani na nje walijiridhisha na kuweza kutoa taarifa juu ya zoezi la uchaguzi kwenda vizuri,kwa nini tume ya uchaguzi iliamua kufuta matokeo ya uchaguzi huo?, je tume imeamua kufanya hivyo kwa maslahi ya nani?,mimi siamini kama matokeo yote yanaweza kuwa na kasoro wakati kuna watu maalum walikuwepo wakisimamia zoezi hilo kuhakikisha linafanyika vizuri. Kama tume imeamua kuchukua uamzi huo kwa maslahi ya watu wachache au chama,itambue kufanya hivyo ni kinyume na demokrasia na nikinyume na katiba,kama tuliamua kuwa nchi ya kidemokrasia na kuruhusu mfumo wa vyama vingi basi hatuna budi kukubaliana na matokeo ya mfumo huo.
Afrika imekuwa na changamoto kubwa hasa linapokuja suala la demokrasia na mfumo wa vyama vingi,vyama tawala vimekuwa vikitumia nguvu dora  kufunja sheria  na kukiuka katiba hasa vinapoonekana kuelekea kushindwa na vyama vya upinzani katika chaguzi,nafikiri hili ndilo limekuwa likipelekea hata matokeo ya uchaguzi kufutwa au kuchelewa kutangazwa kwa baadhi ya vituo vya uchaguzi.Nadhani  vyama tawala vinasahau kuwa wananchi ndiyo wenye nchi,hivyo wakiamua kuchagua chama wanachokiona kwao ni sahihi  hakuna sababu ya kutumia nguvu dora na ukiukwaji wa katiba kwa kupindisha sheria na kumweka mtu ambaye chama tawala kinamtaka,wananchi wameamua hivyo lazima tuheshimu maamuzi yao.Kama wazanzibari wameamua kumchagua wanayemtaka basi tuheshimu maamuzi yao na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.
Baada ya matokeo ya uchaguzi kufutwa ,tume hivi karibuni ilitangaza tarehe ya uchaguzi kurudiwa yaani tarehe 20 Machi,2016.Sikuona sababu ya msingi ya uchaguzi kurudiwa,huu mkwamo wa kisiasa ungeweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya pande mbili kufanyika yaani CCM na CUF.Nikinukuu maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi hivi majuzi katika sherehe za maadhimisho ya Chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 39,”Alisema hakupenda uchaguzi urudiwe”.Nafikiri hiyo ingekuwa fursa  ya pande mbili yaaani CCM na CUF  kutanguliza maslahi ya taifa na mazungumzo kufanyika na hatimaye kufikia muafaka na matokeo kutangazwa.Kurudia  uchaguzi kwanza ni gharama na inaweza kupelekea wazanzibari kutokwa na imani na tume ya uchaguzi na mwisho inaweza kuleta uadui kwa vyama na serikali hasa kwa wananchi kuichukia serikali iliyopo na kuona hakuna sababu ya wao kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa sababu tume haiaminiki tena.
Mimi naamini, endapo Chama Cha Mapinduzi kikiamua kutanguliza maslahi ya taifa mbele basi  suluhu inaweza  kupatikana kwa urahisi,naamini mpaka sasa Chama Cha wananchi CUF kimeonesha ukomavu kwa kutaka suluhu iwepo.Hivyo fursa hiyo itumike vizuri kwa maslahi ya Zanzibar na Jamhuri ya muungano kwa ujumla .
Chagulani,Shabiru
10/2/2016

12/17/2015

Tanzania kutafuta suluhu Burundi?

Nafarijika sana kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimwagiza Waziri wa mambo ya nje kuangalia namna ambavyo mazungumzo yanaweza kufanyika na kufikia muafaka dhidi ya kile kinachoendelea Burundi,naanza kuona ile dhana ya u-Afrika yaani Pan-Afrikanism, nafikiri wale wenye kufahamu falsafa hiyo watakubaliana na mimi kuwa hatuwezi kuwa wa-Afrika kama wenzetu Burundi hawako salama.
           Chagulani,S

12/09/2015

Tunakumbuka na kujifunza nini Desemba 9?

Leo ni tarehe 9/12, ni siku kubwa sana kihistoria kwa Taifa letu.Ni siku ambayo nchi yetu ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni,harakati za kupigania uhuru zikiongozwa na Mwl Julius K.Nyerere,harakati hizo zilianaza punde baada ya vita ya pili ya dunia kwa mataifa ya yaliyokuwa chini ya ukoloni,lengo lilikuwa ni Afrika kuwa huru na waafrika kujitawala wao wenyewe,
Kimsingi, haikuwa kazi ndogo maana wengi waliweza kupoteza uhai kwa maana ya damu kumwagika na kuhakikisha Afrika inakuwa huru.Harakati hizo zilifanikiwa lakini kwa muda mrefu,hivyo lengo lilifankiwa na Afrika kuwa huru na watu wake kuwa huru.Kwa mara ya kwanza baada ya harakati hizo kufanikiwa,waafrika waliweza kijitawala kwa maana ya kuwa viongozi wa nchi na kuanza kujenga nchi zao kwa kutumia rasilimali zilizkuwepo Afrika na kuhakikisha kila mwafrika ananufaika na rasilimali hizo.
Lakini baada ya viongozi hao kutawala na baadae kustaafu tumeshuhudia mambo kutoenda sawa kwa maana ya waliokabidhiwa kijiti kubadilika na kuwa wakoloni weusi na waafrika kuanza kuonekana kama watumwa ndani ya nchi zao,hili linaweza kudhihirishwa na baadhi ya nchi za kiafrika kuwa mambo hayaendi sawa kwa mifumo iliyopo sasa kwa kutokuwepo kwa mgawanyo sawa wa rasilimali na waafrika kutofaidi rasilimali walizobarikiwa.
Wito wangu na kilichopelekea mimi kutoa mtazamo huu ni kuwakumbusha watawala wetu kuwa pale tunaposherekea uhuru,tusisherekee tu kwa gwaride na anasa kwa tabaka tawala bali tukumbuke lengo la kupigania uhuru yaani waafrika kuwa huru na kujitawala na serikali kusimamia rasiliamali zilizopo na kila mwafrika kunufaika na rasilimali hizo na kujenga mataifa yetu kwa ujumla.
         
Chagulani,Shabiru
09.12.2015

7/16/2015

Je,Magufuli atatukomboa?

Je,  Magufuli atatukomboa?
Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi kilikua na vikao ambavyo vilipelekea kumpitisha John Pombe Magufuli kama Mgombea Urais kupitia CCM  katika uchaguzi unaotegemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.  
Kwanza, nachukua fursa hii kumpongeza kwa kupitishwa na kuwa mgombea wa CCM  katika  uchaguzi utakao fanyika mwezi Oktoba,haikuwa kazi  rahisi kufikia uamzi huo lakini kupitia vikao vilivyofanyika kwa muda mrefu hatimaye aliweza kupitishwa.
Leo katika makala haya tunaangalia kama mgombea huyo anaweza kuwa Mwarobaini kwa matatizo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
John Pombe Magufuli  ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, hasa ukizingatia kuwa amekuwa waziri kuanzia awamu ya tatu mpaka awamu ya nne, pia anasikifa kwa kuwa mchapakazi na mtu mwenye maamuzi ya haraka  katika kutafuta ufumbuzi wa jambo lolote.Yote hayo yamedhihirika katika wizara mbalimbali alizozipitia, hivyo ana uzoefu wa masuala mbalimbali katika wizara mbalimbali na utendaji  kwa ujumla.
Kwa mtazamo huu nilioeleza hapo juu, ndugu Magufuli anaonekana kama malaika au mkombozi machoni mwa watu wengi, mtazamo huo unaweza kufanana  na ule wa  watu waliokuwa nao mwaka 2005 kipindi Jakaya Kikwete alipopitishwa na kuanza kufanya kampeini sehemu mbalimbali za nchi, wengi walionekana kummunga mkono wakitegemea kuwa ndiye mkombozi wao, hivyo waliimunga mkono na kuweza kushinda  uchaguzi kwa asilimia kubwa. Hivyo hali hiyo inaweza kujirudia tena  mwaka huu katika uchaguzi.
Ukisoma ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya mwaka  1977  inasema hivi katika vifungu a,b na c ( a)”.Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamalaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” ( b)”.lengo kuu la serikali  litakuwa  ni ustawi wa wananchi” ( c)Serikali itawajibika kwa wananchi. Kwa nukuu ya vifungu hivyo hapo juu, tunaweza kupima kama serikali ya awamu ya nne iliweza kutimiza wajibu wake kikatiba kwa kuhakikisha ustawi wa wananchi wake, kwanza katika; afya, maji, elimu, umeme na miundombinu. Nafikiri wewe  msomaji wa makali hii unaweza  kujua hali halisi ilivyo katika sekta ya afya ambapo ni rahisi kwenda hospitali ukaambiwa hakuna dawa wala vifaa tiba hali ambayo imekuwa ikiipelekea vifo hasa  kwa mama wajawazito na watoto,  pili sote tunafahamu kuwa  maji bado ni tatizo mijini na vijijini, elimu nayo inayotolewa  sio bora na inafahamika uwepo wa changamoto mablimbali kt sekta ya elimu. Changamoto hizo tumekumbana nazo ktk awamu ya nne kwa kipindi cha miaka kumi chini ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi kilichotoa ahadi ya “Maisha Bora kwa kila Mtanzania.”
Naamini Magufuli haya yote anayajua vizuri maana amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka ishirini, pia ni miongoni mwa wabunge  walioshuhudia  matukio ya ufisadi toka awamu ya tatu  mpaka ya nne, lkn alishiriki katika bunge maalum la katiba na kuweza kupitisha katiba pendekezwa  ya CCM na kupuuza ile iliyokuwa imependekezwa na wananchi.Je mnawezaje kumpa ridhaa mtu huyu ambaye anaamini katika maslahi ya chama kwanza kuliko taifa?.
Nafikiri ifike pahala watanzania  tuache ugonjwa wa kusahau tuliyoyapitia ktk awamu ya nne.Tutakuwa tunajidanganya kutegemea  ukombozi wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya taifa kupitia Chama Cha  Mapinduzi, tumeshuhudia mengi bungeni ambapo wabunge walionekana wapo tayari kutetea uovu  kwa vijembe na kejeli kwa maslahi ya chama, pili wamekuwa tayari kufanyanya lolote hata kama linakiuka sheria kanuni na utaratibu ili kutimiza maslahi ya chama bila kujali lolote linazoweza kujitokeza na kuathiri uchumi wa taifa,hii inaweza kudhihirishwa na utetezi wa wabunge wa CCM ktk skendo ya escrow,pia tumeshuhudia miswada ya gesi na mafuta ikipitishwa akidi bila kutia na wadau mbali mbali bila kushirikishwa na miswada kutojadiliwa kwa kina.
Kwa kuhitimisha, Chama Cha Mapinduzi hakipo tayari kumkoboa mwananchi na kuhakikisha ustawi wake na Taifa  kwa ujumla.Miaka kumi inayoelekea ukomo wake Oktoba inaweza kusaidia katika kufanya tathimini.Tuna mengi yakujifunza kwa kufanya maamuzi kama wenzetu Kenya na Nigeria walivyofanya.
Kura yako ni silaha yako, itumie vizuri
Chagulani, Shabie

4/14/2015

: PITIA TAARIFA YA (CAG) ILIYOPELEKEA MEYA ANATORY A...

 : PITIA TAARIFA YA (CAG) ILIYOPELEKEA MEYA ANATORY A...: Pichani ni    Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG )    Bw. Ludovick S. L. Utouh.     Mwanzo wa taarifa. Waziri mkuu alit...