Je, serikali inawajibika?
Serikali katika misingi ya kidemokrasia ujipatia viongozi wake kupitia uchaguzi unaofanyika sehemu
husika.Viongozi hao wanaochagulia ndio baadae utengeneza serikali katika ngazi
mbalimbali ili kuweza kutimiza majukumu ya kiserikali.Viongozi hawa ndiyo wanaokua
wawakilishi wa wananchi katika shughuli mbalimbali za kiserikali, pia Kiongozi
kama rais naye ufanya uteuzi wa watu
mbalimbali ili waweze kumsaidia katika idara mbalimbali kiutendaji ili kuweza kufikia malengo kwa maendeleo na ustawi wa nchi
husika.
Hivyo serikali
yenye kujua na kutambua wajibu wake ujikita zaidi kwa kuwajibika ili kuweza kuhudumia wananch kwa kutumia
rasilimali ilizonazo na kuwahakikishia ustawi uliokua mzuri kimaisha.Hivyo
wananchi ujenga imani na serikali yao kwa
kuona serikali ikiwahakikishia ustawi wao katika Nyanja mbalimbali kama
za kijamii na kiuchumi.
Na serilikali
zilizokua makini na zenye malengo ya dhati hutekeleza majukumu yao kwa kuhakiki
wananchi mfano wafanya biashara wanapata mazingira mazuri yakuwezewsha biashara
hizo kufanyika kwa urahisi na mazingira rafiki, hivyo watu hawa uweza kujipatia
kipato kupitia biashara zao na kuweza kuendesha familia zao na pia serikali
ukusanya kodi kwa wafanya biashara hawa.
Kodi inayopatikana
kama mapato hutumiwa na serikali katika kuendesha shughuli zake kwa kutoa
huduma kwa wanachi mfano kama upatikanaji wa vifaa tiba na mdawa
hospitalini ili kuweza kuhudumia wagonjwa kwa kuhakikisha huduma za afya
zinapatikana kwa urahisi.vilevile
wananchi watataraji kupata huduma za maji ili kuweza kurahisisha shughuli
zao na pia watatarajia serikali inahakikisha uwepo wa elimu bora kwa uwepo wa
watalam, mazingira bora yakufundishia na vifaa bora vya kufundishia .
Upatikanji
wa huduma hizo muhimu kwa wananchi utekelezwa na serilali yenye ni ya dhati
kuona taifa linapiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali .lakini kwetu
hapa mambo yamekua tofauti na jinsi wananchi walivyotaraji kua uwepo wa
serikali madarakani kuwa ni heri kwa mfano baada ya uchaguzi kufanyika serikali
uonekana kama vile inasahau wajibu wake mfano katika elimu mazingira ya
kufundishia saio rafiki, vifaa vya kufundishia hakuna hali hii upelekea utendaji kazi katika sehumu
hiyo kuwa mgumu na hatimaye ufaulu ushuka na elimu pia ushuka hili lipo wazi
kwa matokeo ya kidato cha nnea yaliyopita yalikua mabaya na hatujaona hatua
zilizochukuliwa ili kutatua tatizo hili.
Katika afya pia huduma bado ni duni hasa
katika upatikanaji kwa maana ya vituo kuwa
mbali hasa maeneo ya vijijini ambapo wananchi ulazimika kutembea umbali
mrefu kili kuweza kupata huduma .Na hata
wakifika vifaa tiba hakuna hivyo hali hii upelekea vifo hasa kwa mama
wajawazito wanaotembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo huko vijijni,na mijini
vuilevile huduma ni duni madawa na watalaam
hakuna hii nayo uwafanya wataalam kutofika vituo vya kazi maana mazingira sio
rafiki na hatimaye kimbilio lao ni nje ya nchi. Mfano Botswana ndio limekua
kimbilio la madaktali wengi kutoka Tanzania.
Upatikanaji wa
maji nalo ni kero kwa wanachi mijini na vijijini pia. Vijijini watu usafiri
umbali mrefu wakati wa usiku hasa akina
mama ili kuweza kupata maji kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za
nyumbani.MIjini pia maji nayo ni ya mgao na sehemu nyingine hayapatikani kabisa
wananchi ulazimika wakati mwingine
kununua maji kwa gharama kubwa,kutopatikana kwa maji upelekea kukwama kwa
shughuli za uzalishaji hata za nyumabani pia,tatizo hili lipo maeneo mengi hasa
Dar es salaam,Morogoro,Singida na
Dodoma.
Umasikini nao
umezidi kuongezeka kwa wananchi kila kukicha.Hi inatokana na serikali kutotumia
rasilimali ilizonazo ili kuwatengeneza wananchi fursa ili nao waweze kujiinua
kimaisha, na badala ake serikali kuwanyanyasa wananchi pale wanapojishughulisha
kwa kuanzisha biasharara ndogondogo kwa
kuwatoza kodi bila kuwaboreshea mazingira salama kwa ajili ya kuendesha
shughuli zao na wakati mwingine wajasiriamali hao ufukuzwa na serikali bila
hata kutafutiwa sehemu nyingine ya kuweza kueendeshea buiashara zao. Hali
upelekea watu kutokua na uhakika hata wa kupata kipato cha kuweza kumudu maisha yao
Ni jukumu la
serikali kuakikisha wananchi na mali zao wanakua salama kupitia mamlaka
zake.Kwetu hapa usalama wa raia uko mashakani
hii ipo wazi na linadhihirishwa na matukio mengi ambayo yamekua
yakitokea hapa nchini watu kupotza uhai na hata mali zao pia, mfano hivi majuzi
tumempoteza Dr Sengondo Mvungi aliyevamiwa nyumbani kwake huko kibamba. Pia malalamiko mengi yamekua yakitolewa juu ya
utendaji wa jeshi la polisi kukamata watu ovyo na pengine mtu kutosikilizwa na
hatimae jeshi la polisi ufikia uamzi wa kufanyanya lolote lile kwa jinsi litakavyo
dhidi ya raia.
Serikali makini
kote duniani ukemea vikali masuala ya rushwa. Hapa kwetu ni tofauti kidogo kwa
maana ya mamlaka husika uonekana kua wakali kwa matukio madogo madogo ya rushwa
lakini mamlaka hizi ushindwa kutekeleza wajibu wake pale tuhuma za rushwa dhidi
ya viongozi wa umma zinapotokea na hatua uchukua muda mrefu kuchukuliwa kwa
kisingizio cha uchunguzi unafanyika . Mfano
tuhuma mbalimbali zimekua kikitolewa juu ya baadhi ya viongozi wa serikali lakini hakuna chochote kinachofanyika .Hali
hii upelekea kushamiri kwa vitendo hivyo kama ilivyo sasa.
Serikali makini inapopata ridhaa ya kuwa madarakani, jukumu
lake kubwa ni kuhakikisha ustawi wa
wananchi wake unakua bora ili kuweza
kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote na sio kufikiria uchaguzi mwingine
pale wanapo pewa na ridhaa na wananchi.
Chagulani Shabiru
Mwanza, Tanzania
2014