12/17/2015

Tanzania kutafuta suluhu Burundi?

Nafarijika sana kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimwagiza Waziri wa mambo ya nje kuangalia namna ambavyo mazungumzo yanaweza kufanyika na kufikia muafaka dhidi ya kile kinachoendelea Burundi,naanza kuona ile dhana ya u-Afrika yaani Pan-Afrikanism, nafikiri wale wenye kufahamu falsafa hiyo watakubaliana na mimi kuwa hatuwezi kuwa wa-Afrika kama wenzetu Burundi hawako salama.
           Chagulani,S

12/09/2015

Tunakumbuka na kujifunza nini Desemba 9?

Leo ni tarehe 9/12, ni siku kubwa sana kihistoria kwa Taifa letu.Ni siku ambayo nchi yetu ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni,harakati za kupigania uhuru zikiongozwa na Mwl Julius K.Nyerere,harakati hizo zilianaza punde baada ya vita ya pili ya dunia kwa mataifa ya yaliyokuwa chini ya ukoloni,lengo lilikuwa ni Afrika kuwa huru na waafrika kujitawala wao wenyewe,
Kimsingi, haikuwa kazi ndogo maana wengi waliweza kupoteza uhai kwa maana ya damu kumwagika na kuhakikisha Afrika inakuwa huru.Harakati hizo zilifanikiwa lakini kwa muda mrefu,hivyo lengo lilifankiwa na Afrika kuwa huru na watu wake kuwa huru.Kwa mara ya kwanza baada ya harakati hizo kufanikiwa,waafrika waliweza kijitawala kwa maana ya kuwa viongozi wa nchi na kuanza kujenga nchi zao kwa kutumia rasilimali zilizkuwepo Afrika na kuhakikisha kila mwafrika ananufaika na rasilimali hizo.
Lakini baada ya viongozi hao kutawala na baadae kustaafu tumeshuhudia mambo kutoenda sawa kwa maana ya waliokabidhiwa kijiti kubadilika na kuwa wakoloni weusi na waafrika kuanza kuonekana kama watumwa ndani ya nchi zao,hili linaweza kudhihirishwa na baadhi ya nchi za kiafrika kuwa mambo hayaendi sawa kwa mifumo iliyopo sasa kwa kutokuwepo kwa mgawanyo sawa wa rasilimali na waafrika kutofaidi rasilimali walizobarikiwa.
Wito wangu na kilichopelekea mimi kutoa mtazamo huu ni kuwakumbusha watawala wetu kuwa pale tunaposherekea uhuru,tusisherekee tu kwa gwaride na anasa kwa tabaka tawala bali tukumbuke lengo la kupigania uhuru yaani waafrika kuwa huru na kujitawala na serikali kusimamia rasiliamali zilizopo na kila mwafrika kunufaika na rasilimali hizo na kujenga mataifa yetu kwa ujumla.
         
Chagulani,Shabiru
09.12.2015

7/16/2015

Je,Magufuli atatukomboa?



Je,  Magufuli atatukomboa?
Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi kilikua na vikao ambavyo vilipelekea kumpitisha John Pombe Magufuli kama Mgombea Urais kupitia CCM  katika uchaguzi unaotegemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.  
Kwanza, nachukua fursa hii kumpongeza kwa kupitishwa na kuwa mgombea wa CCM  katika  uchaguzi utakao fanyika mwezi Oktoba,haikuwa kazi  rahisi kufikia uamzi huo lakini kupitia vikao vilivyofanyika kwa muda mrefu hatimaye aliweza kupitishwa.
Leo katika makala haya tunaangalia kama mgombea huyo anaweza kuwa Mwarobaini kwa matatizo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
John Pombe Magufuli  ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, hasa ukizingatia kuwa amekuwa waziri kuanzia awamu ya tatu mpaka awamu ya nne, pia anasikifa kwa kuwa mchapakazi na mtu mwenye maamuzi ya haraka  katika kutafuta ufumbuzi wa jambo lolote.Yote hayo yamedhihirika katika wizara mbalimbali alizozipitia, hivyo ana uzoefu wa masuala mbalimbali katika wizara mbalimbali na utendaji  kwa ujumla.
Kwa mtazamo huu nilioeleza hapo juu, ndugu Magufuli anaonekana kama malaika au mkombozi machoni mwa watu wengi, mtazamo huo unaweza kufanana  na ule wa  watu waliokuwa nao mwaka 2005 kipindi Jakaya Kikwete alipopitishwa na kuanza kufanya kampeini sehemu mbalimbali za nchi, wengi walionekana kummunga mkono wakitegemea kuwa ndiye mkombozi wao, hivyo waliimunga mkono na kuweza kushinda  uchaguzi kwa asilimia kubwa. Hivyo hali hiyo inaweza kujirudia tena  mwaka huu katika uchaguzi.
Ukisoma ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ya mwaka  1977  inasema hivi katika vifungu a,b na c ( a)”.Wananchi ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamalaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” ( b)”.lengo kuu la serikali  litakuwa  ni ustawi wa wananchi” ( c)Serikali itawajibika kwa wananchi. Kwa nukuu ya vifungu hivyo hapo juu, tunaweza kupima kama serikali ya awamu ya nne iliweza kutimiza wajibu wake kikatiba kwa kuhakikisha ustawi wa wananchi wake, kwanza katika; afya, maji, elimu, umeme na miundombinu. Nafikiri wewe  msomaji wa makali hii unaweza  kujua hali halisi ilivyo katika sekta ya afya ambapo ni rahisi kwenda hospitali ukaambiwa hakuna dawa wala vifaa tiba hali ambayo imekuwa ikiipelekea vifo hasa  kwa mama wajawazito na watoto,  pili sote tunafahamu kuwa  maji bado ni tatizo mijini na vijijini, elimu nayo inayotolewa  sio bora na inafahamika uwepo wa changamoto mablimbali kt sekta ya elimu. Changamoto hizo tumekumbana nazo ktk awamu ya nne kwa kipindi cha miaka kumi chini ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi kilichotoa ahadi ya “Maisha Bora kwa kila Mtanzania.”
Naamini Magufuli haya yote anayajua vizuri maana amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka ishirini, pia ni miongoni mwa wabunge  walioshuhudia  matukio ya ufisadi toka awamu ya tatu  mpaka ya nne, lkn alishiriki katika bunge maalum la katiba na kuweza kupitisha katiba pendekezwa  ya CCM na kupuuza ile iliyokuwa imependekezwa na wananchi.Je mnawezaje kumpa ridhaa mtu huyu ambaye anaamini katika maslahi ya chama kwanza kuliko taifa?.
Nafikiri ifike pahala watanzania  tuache ugonjwa wa kusahau tuliyoyapitia ktk awamu ya nne.Tutakuwa tunajidanganya kutegemea  ukombozi wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya taifa kupitia Chama Cha  Mapinduzi, tumeshuhudia mengi bungeni ambapo wabunge walionekana wapo tayari kutetea uovu  kwa vijembe na kejeli kwa maslahi ya chama, pili wamekuwa tayari kufanyanya lolote hata kama linakiuka sheria kanuni na utaratibu ili kutimiza maslahi ya chama bila kujali lolote linazoweza kujitokeza na kuathiri uchumi wa taifa,hii inaweza kudhihirishwa na utetezi wa wabunge wa CCM ktk skendo ya escrow,pia tumeshuhudia miswada ya gesi na mafuta ikipitishwa akidi bila kutia na wadau mbali mbali bila kushirikishwa na miswada kutojadiliwa kwa kina.
Kwa kuhitimisha, Chama Cha Mapinduzi hakipo tayari kumkoboa mwananchi na kuhakikisha ustawi wake na Taifa  kwa ujumla.Miaka kumi inayoelekea ukomo wake Oktoba inaweza kusaidia katika kufanya tathimini.Tuna mengi yakujifunza kwa kufanya maamuzi kama wenzetu Kenya na Nigeria walivyofanya.
Kura yako ni silaha yako, itumie vizuri
Chagulani, Shabie

4/14/2015

: PITIA TAARIFA YA (CAG) ILIYOPELEKEA MEYA ANATORY A...

 : PITIA TAARIFA YA (CAG) ILIYOPELEKEA MEYA ANATORY A...: Pichani ni    Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali ( CAG )    Bw. Ludovick S. L. Utouh.     Mwanzo wa taarifa. Waziri mkuu alit...

Read the petition below then sign it

https://secure.avaaz.org/en/petition/President_of_the_United_Republic_of_Tanzania_Hon_Jakaya_Kiwete_To_consider_not_signing_the_two_laws_pending_enabling_ame/?copy

3/31/2015

3/18/2015

Je,serikali inawajibika?



                                                   Je,  serikali inawajibika?
Serikali katika misingi ya kidemokrasia  ujipatia viongozi  wake kupitia uchaguzi unaofanyika sehemu husika.Viongozi hao wanaochagulia ndio baadae utengeneza serikali katika ngazi mbalimbali ili kuweza kutimiza majukumu ya kiserikali.Viongozi hawa ndiyo wanaokua wawakilishi wa wananchi katika shughuli mbalimbali za kiserikali, pia Kiongozi kama rais naye ufanya uteuzi  wa watu mbalimbali ili waweze kumsaidia katika idara mbalimbali kiutendaji ili kuweza  kufikia malengo kwa maendeleo na ustawi wa nchi husika.
      Hivyo serikali yenye kujua na kutambua wajibu wake ujikita zaidi kwa kuwajibika  ili kuweza kuhudumia wananch kwa kutumia rasilimali ilizonazo na kuwahakikishia ustawi uliokua mzuri kimaisha.Hivyo wananchi ujenga imani na serikali yao kwa  kuona serikali ikiwahakikishia ustawi wao katika Nyanja mbalimbali kama za kijamii na kiuchumi.
       Na serilikali zilizokua makini na zenye malengo ya dhati hutekeleza majukumu yao kwa kuhakiki wananchi mfano wafanya biashara wanapata mazingira mazuri yakuwezewsha biashara hizo kufanyika kwa urahisi na mazingira rafiki, hivyo watu hawa uweza kujipatia kipato kupitia biashara zao na kuweza kuendesha familia zao na pia serikali ukusanya kodi kwa wafanya biashara hawa.
    Kodi inayopatikana kama mapato hutumiwa na serikali katika kuendesha shughuli zake kwa kutoa huduma kwa wanachi  mfano  kama upatikanaji wa vifaa tiba na mdawa hospitalini ili kuweza kuhudumia wagonjwa kwa kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi.vilevile  wananchi watataraji kupata huduma za maji ili kuweza kurahisisha shughuli zao na pia watatarajia serikali inahakikisha uwepo wa elimu bora kwa uwepo wa watalam, mazingira bora yakufundishia na vifaa bora vya kufundishia .
          Upatikanji wa huduma hizo muhimu kwa wananchi utekelezwa na serilali yenye ni ya dhati kuona taifa linapiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali .lakini kwetu hapa mambo yamekua tofauti na jinsi wananchi walivyotaraji kua uwepo wa serikali madarakani kuwa ni heri kwa mfano baada ya uchaguzi kufanyika serikali uonekana kama vile inasahau wajibu wake mfano katika elimu mazingira ya kufundishia saio rafiki, vifaa vya kufundishia hakuna  hali hii upelekea utendaji kazi katika sehumu hiyo kuwa mgumu na hatimaye ufaulu ushuka na elimu pia ushuka hili lipo wazi kwa matokeo ya kidato cha nnea yaliyopita yalikua mabaya na hatujaona hatua zilizochukuliwa ili kutatua tatizo hili.
        Katika afya pia huduma bado ni duni hasa katika upatikanaji kwa maana ya vituo kuwa  mbali hasa maeneo ya vijijini ambapo wananchi ulazimika kutembea umbali mrefu kili kuweza kupata huduma  .Na hata wakifika vifaa tiba hakuna hivyo hali hii upelekea vifo hasa kwa mama wajawazito wanaotembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo huko vijijni,na mijini vuilevile huduma ni duni  madawa na watalaam hakuna hii nayo uwafanya wataalam kutofika vituo vya kazi maana mazingira sio rafiki na hatimaye kimbilio lao ni nje ya nchi. Mfano Botswana ndio limekua kimbilio la madaktali wengi kutoka Tanzania.
    Upatikanaji wa maji nalo ni kero kwa wanachi mijini na vijijini pia. Vijijini watu usafiri umbali mrefu  wakati wa usiku hasa akina mama ili kuweza kupata maji kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za nyumbani.MIjini pia maji nayo ni ya mgao na sehemu nyingine hayapatikani kabisa wananchi ulazimika  wakati mwingine kununua maji kwa gharama kubwa,kutopatikana kwa maji upelekea kukwama kwa shughuli za uzalishaji hata za nyumabani pia,tatizo hili lipo maeneo mengi hasa Dar es  salaam,Morogoro,Singida na Dodoma.
       Umasikini nao umezidi kuongezeka kwa wananchi kila kukicha.Hi inatokana na serikali kutotumia rasilimali ilizonazo ili kuwatengeneza wananchi fursa ili nao waweze kujiinua kimaisha, na badala ake serikali kuwanyanyasa wananchi pale wanapojishughulisha kwa kuanzisha  biasharara ndogondogo kwa kuwatoza kodi bila kuwaboreshea mazingira salama kwa ajili ya kuendesha shughuli zao na wakati mwingine wajasiriamali hao ufukuzwa na serikali bila hata kutafutiwa sehemu nyingine ya kuweza kueendeshea buiashara zao. Hali upelekea watu kutokua na uhakika hata wa kupata kipato  cha kuweza kumudu maisha yao
       Ni jukumu la serikali kuakikisha wananchi na mali zao wanakua salama kupitia mamlaka zake.Kwetu hapa usalama wa raia uko mashakani  hii ipo wazi na linadhihirishwa na matukio mengi ambayo yamekua yakitokea hapa nchini watu kupotza uhai na hata mali zao pia, mfano hivi majuzi tumempoteza Dr Sengondo Mvungi aliyevamiwa nyumbani kwake huko kibamba. Pia  malalamiko mengi yamekua yakitolewa juu ya utendaji wa jeshi la polisi kukamata watu ovyo na pengine mtu kutosikilizwa na hatimae jeshi la polisi ufikia uamzi wa kufanyanya lolote lile kwa jinsi litakavyo dhidi ya raia.
     Serikali makini kote duniani ukemea vikali masuala ya rushwa. Hapa kwetu ni tofauti kidogo kwa maana ya mamlaka husika uonekana kua wakali kwa matukio madogo madogo ya rushwa lakini mamlaka hizi ushindwa kutekeleza wajibu wake pale tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi wa umma zinapotokea na hatua uchukua muda mrefu kuchukuliwa kwa kisingizio cha uchunguzi  unafanyika . Mfano tuhuma mbalimbali zimekua kikitolewa juu ya baadhi ya viongozi wa serikali  lakini hakuna chochote kinachofanyika .Hali hii upelekea kushamiri kwa vitendo hivyo kama ilivyo sasa.
Serikali makini inapopata ridhaa ya kuwa madarakani, jukumu lake kubwa ni kuhakikisha  ustawi wa wananchi wake unakua bora  ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote na sio kufikiria uchaguzi mwingine pale wanapo pewa na ridhaa na wananchi.
   Chagulani Shabiru
   Mwanza, Tanzania
2014

Je kodi inakusanywa ipasavyo ili kuleta maendeleo?



                            Je kodi inakusanywa ipasavyo ili kuleta maendeleo?
Ni dhahiri kua serikali yoyote duniani ili iweze kuendeshwa lazima ihakikishe wananchi wanalipa kodi mbalimbali kuwezesha  shughuli za serikali kufanyika, ikiwemo kuhudumia wananchi wake katika huduma mbalimbali mfano maji,afya,elimu na kadhalika .
Ni miezi mitatu  imepita kodi ya laini ya simu(sim card tax) imepitishwa na serikali, na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  imeziandikia barua kampuni za simu kuzitaka  kuanza kukata kodi hiyo kwa kila mtumiaji mwenye laini ya simu,hivyo ( TRA ) imeagiza kukata kodi kuanzia mwezi wa saba mpaka  sasa kwa maana  mwananchi hana budi kulipa shillingi elfu tatu .Taifa lolote ili liendelee lazima likusanye kodi kama vyanzo vya mapato katika kuendesha shughuli mbalimbali za serikali hivyo kila mwananchi hana wajibu wa kulipa kodi kwa maana ya kuwa mfanyakazi ,mfanyabiashara kutokana na biashara au kazi afanyayo na kodi nyingine ukusanywa na kulipwa kupitia manunuzi ya bidhaa mbalimbali .
   Mapato yanayokusanywa na serikali  kupitia kodi mbalimbali  serikali haina budi kuyarudisha kwa wananchi  kwa kuhakikissha wananchi  wanapata huduma bora katika elimu,maji , afya na huduma nyingine. Mfano kupitia kodi inayokusanywa na serikali  tunategemea  katika vituo vya afya  madawa na vifaa tiba viwepo ili kuwezesha wananchi kupata matibabu kwa urahisi  lakini kwetu hapa huduma zimeendelea kuwa duni kila kukicha hasa maeneo ya vijijini  kutokana na  mamlaka husika kutotekeleza wajibu wake katika ukusanyaji wa kodi kama vyanzo vya mapato kwa serikali.
 Hali hii ya kutokuwepo dhana ya uwajibikaji katika mamlaka husika zilizopewa dhamana ya kuhakikisha kodi inalipwa inapelekea wafanyabiashara wakubwa na hata  makapuni makubwa kutokulipa kodi  ipasavyo na hata yakilipa kodi ni kwa kiasi kidodo ukilinganisha ukubwa na uzalishaji wa makampuni hayo, na wafanya biashara wadogowadogo wamekua wakilipa kodi lakini hawatengezewi miundo mbinu itakayowawezesha  biashara yao kua endelevu na hatimae hunyanyaswa kwa  kufungiwa biashara zao na wakati mwingine uendesha shughuli zao katika mazingira yasiyo rafiki
  Wakati mwingine umekuwepo misamaha ya kodi  kwa makampuni tajiri  ya madini wakati makampuni haya yamekua yakipata faida kubwa sana kupita kiasi na kukataa kueleza wazi mapato wanayoyapata mfano  makapumpuni ya simu yamekua hayalipi kodi inayotakiwa ukilinganisha na faida inayopatikana kupitia mitandao hiyo ya simu.
         Hali hii inatokana na mamlaka husika kutotokeleza wajibu wake ipasavyo  na kutokuwepo kwa uadilifu katika ukusanyaji wa mapato hasa kwa makampuni makubwa kama ya simu na migodi pale maafisa wa mamlaka hizo wanapotengewa kiasi kikubwa cha fedha na makampuni hayo na hatimae kiasi kidogo ukusanywa na mwisho wa siku mzigo uelekezwa kwa mwanachi wa kawaida( mlalahoi)   asiyekua na uhakika wa kupata hata  milo miwili kwa siku,mwananchi huyu atake asitake lazima alipie kadi ya simu yake kwa kila mwezi kama serikali ilivyoelekeza kupitia mamlaka ya mapato Tanzania.inasikitisha sana kuona wafanyabiashara wakubwa wenye kumiliki makampuni makubwa pia  wanakwepa kulipa kodi kutokana na ushawishishi wa kifedha walio nao .
  Serikali za  mataifa yaliyoendelea duniani yamejidhatiti zaidi katika ukusaji wa kodi kwa uadilifu na uzalendo ili kuweza kupata mapato yatakayowezesha serikali kuboresha huduma za jamii kwa wananchi wake lakini kwetu hapa wajanja wachache wamejidhatiti katika kukwepa kodi na kuruhusu mianya ya rushwa ili zoezi la  ukusanyaji wa kodi  kutofanyika kama inavyotakiwa na hali hii huzolotesha kasi ya maendeleo kwa taifa  pale serikali inapojikuta ikikopa  pesa nje kwa ajili ya bajeti.
     Chagulani Shabiru
    Mwanza,Tanzania
    2014



                                            
                    Tusitarajie katiba mpya kwa sasa
 Katiba ni mwongozo wenye sheria na kanuni mbalimbali kwa ajili ya uendeshaji wa nchi.Mataifa yaliyo makini duniani uruhusu   utaratibu uliokuwa bora kwa kuwashirikisha wananchi katika upatikanaji wa katiba kwa kukusanya maoni yao na kuyafanyia uchambuzi kupitia tume na kisha katiba kutungwa kwa kuzingatia maoni yaliyopendekezawa na wananchi.

Katika mchakato wa kutafuta katiba mpya mh rais aliteua tume iliyokusanya maoni na kuyafanyia uchambuzi wa kina na badae likawepo bunge maalum la katiba ambalo lilijumuisha wajumbe mbali mbali  kama wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao walipatikana kwa sheria iliyopitishwa na bunge nao kuwa sehemu ya bunge maalum la katiba, na wajumbe wengine ni kutoka vyama vya siasa,asasi zisizo za kiraia  ambao waliteuliwa na Rais.

Baada ya uteuzi wa wajumbe wa bunge maalum la katiba ,kazi yao kubwa  ilikua ni kusimamia rasimu kwa kujadili maoni yaliyotolewa na wananchi na kuyaboresha  pia. Suala la kusimamia maoni ya wananchi kwenye rasimu linaonekana kutozingatiwa, hili linadhihirishwa  kwa baadhi ya vifungu vilivyoko kwenye rasimu kuodolewa ,mfano ni kifungu kilichokuwa kikizungumzia tunu za taifa ambazo ni uadilifu,uzalendo na uwajibikaji.Kifungu hiki kimepuuzwa na wajumbe kutoka chama tawala, na hali hiyo ilipelekea umoja  wa katiba ya wananchi ( UKAWA) na baadhi ya wajumbe wengine kutoka bungeni kwa kutoridhiswa na mwenendo wa bunge .
Na kuanza kwa awamu ya pili kwa bunge maalum la katiba kumetiliwa shaka hasa ukizingatia baadhi ya wajumbe waliotoka nje hapo awali, kwa kutoridhishwa na jinsi bunge lilivyokuwa likifanya kazi na jitihada za kuhakikisha wajumbe hao kurejea bungeni zikigonga mwamba kutokana na kutofikiwa kwa maridhiano kwa pande  zote mbili,Hali hii imepelekea upande mmoja yaani wajumbe ambao ni sehemu kubwa ya Chama cha Mapinduzi wao kuonekana ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha katiba inapatikana.
Uwepo huu wa idadi kubwa ya wajumbe ambao ni sehumu ya chama tawala kuendelea na bunge maalum unatiliwa shaka,hii nikutokana wajumbe hao kuondoa kifungu cha wananchi kuwajibisha mbunge na ukomo wa ubunge,kitendo hiki kinaashiria wajumbe kulinda maslahi binafsi kwa kushindwa kusimamia maoni ya wananchi kwa kuyaboresha na badala yake wanaondoa vifungu ambavyo vinaonekana kwao vinaweza kuwa havina maslahi,kufanya hivi ni kinyume na jukumu la bunge maalum la katiba.
Kwa hatua hii bunge kutawaliwa na hisia na kushindwa kujikita katika kujadili maoni ya wananchi ni kiashiria tosha kuwa uwezekano wa kupata katiba bora  iliyotokana na maoni ya wananchi ni mdogo,hii ni kutokana na hali halisi inayoendelea kwa baadhi ya wajumbe kuwa nje ya bunge na mjadala ukiendelea bungeni na waliobaki bungeni kutotimiza majukumu yao na badala yake mchakato kutekwa na msimamo wa chama na wakati mwingine hali hii kuonekana kama fursa kwa baadhi ya wajumbe kama washindi ( winners) kwa kuendelea kubaki bungeni na walioondoka kuonekana kama  walioshindwa ( losers)
Na historia inaonyesha  udhaifu wa bunge letu kutumia wingi wao kufanya maamuzi hata kama hayana tija kwa wananchi ilimradi yana maslahi kwa chama kinachounda serikali, hivyo hii dhana ya winners na losers inaweza kupelekea maamuzi kufanyika  vibaya ilimradi yaa tija kwa watawala,nadhani ungekuwa wakati mzuri sasa kwa kujifunza  kutoka kwa majirani zetu kama Kenya walioweka tofauti zao pembeni na kutanguliza maslahi ya taifa mbele katika upatikanaji wa katiba.
Mwisho kabisa,upatikanaji wa katiba ni maridhiano kwa kuweka misimamo ya vyama pembeni na kusimamia rasimu iliyotokana na maoni yalitolewa na wananchi na itakayodumu kwa miaka mingi ijayo .kutopatikana kwa katiba itakuwa  ni matumizi mabaya  ya fedha za wananchi zilizotumika kuendesha bunge na kulipa posho  wajumbe, na wananchi watakuwa hawajatendewa haki kwa pesa zao kutumika vibaya .
Chagulani Shabiru

Kutoka St. Augustine, Mwanza.
2014