Leo ni tarehe 9/12, ni siku kubwa sana kihistoria kwa Taifa letu.Ni siku
ambayo nchi yetu ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni,harakati za
kupigania uhuru zikiongozwa na Mwl Julius K.Nyerere,harakati hizo
zilianaza punde baada ya vita ya pili ya dunia kwa mataifa ya yaliyokuwa
chini ya ukoloni,lengo lilikuwa ni Afrika kuwa huru na waafrika
kujitawala wao wenyewe,
Kimsingi, haikuwa kazi ndogo maana wengi waliweza
kupoteza uhai kwa maana ya damu kumwagika na kuhakikisha Afrika inakuwa
huru.Harakati hizo zilifanikiwa lakini kwa muda mrefu,hivyo lengo lilifankiwa
na Afrika kuwa huru na watu wake kuwa huru.Kwa mara ya kwanza baada ya
harakati hizo kufanikiwa,waafrika waliweza kijitawala kwa maana ya kuwa
viongozi wa nchi na kuanza kujenga nchi zao kwa kutumia rasilimali
zilizkuwepo Afrika na kuhakikisha kila mwafrika ananufaika na rasilimali
hizo.
Lakini baada ya viongozi hao kutawala na baadae kustaafu
tumeshuhudia mambo kutoenda sawa kwa maana ya waliokabidhiwa kijiti
kubadilika na kuwa wakoloni weusi na waafrika kuanza kuonekana kama watumwa ndani
ya nchi zao,hili linaweza kudhihirishwa na baadhi ya nchi za kiafrika
kuwa mambo hayaendi sawa kwa mifumo iliyopo sasa kwa kutokuwepo kwa
mgawanyo sawa wa rasilimali na waafrika kutofaidi rasilimali
walizobarikiwa.
Wito wangu na kilichopelekea mimi kutoa mtazamo huu ni
kuwakumbusha watawala wetu kuwa pale tunaposherekea uhuru,tusisherekee
tu kwa gwaride na anasa kwa tabaka tawala bali tukumbuke lengo la
kupigania uhuru yaani waafrika kuwa huru na kujitawala na serikali
kusimamia rasiliamali zilizopo na kila mwafrika kunufaika na rasilimali
hizo na kujenga mataifa yetu kwa ujumla.
Chagulani,Shabiru
09.12.2015