2/25/2016

Uganda na Ulaghai katika Demokrasia

Siku ya Alhamis  tarehe 18.2.2016 ni moja ya siku iliyokuwa ya kihistoria nchini Uganda,nahiita siku hiyo ya kistoria kwa sababu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo siku hiyo.Ulikuwa ni uchaguzi wa kihistoria kwa sababu mbalimbali; mosi, ni uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa kutokana na wagombea urais yaani wagombea watatu kukubalika mno  na kuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi,na wagombea hao ni Yoweri Kaguta Museveni  wa chama cha NRM,Dk Kiiza Besigye wa FDC na Amama Mbabazi.Pili ni uchaguzi uliotanguliwa na mdahalo wa wagombea urais kipindi cha kampeini  ambapo kila mmoja wao alijieleza nini angefanya kama angepewa ridhaa na wananchi
Ni dhahiri watu wengi walikuwa na shauku ya kutakakjua na kuona jinsi zoezi zima la uchaguzi litakavyoenda,hiyo inaweza kudhihirishwa na vyombo vya habari kutoka ndani na nje jinsi vlivyomulika zoezi zima la uchaguzi  na pia mitandao ya kijamii nayo haikuwa nyuma kuhakikisha watu wanapashana habari  katika zoezi hilo
Naweza kusema ni uchaguzi uliogubikwa na matukio mengi mpaka kutiliwa shaka kwa jinsi zoezi lilivyoendeshwa na mambo mbalimbali yaliyojitokeza kipindi cha uchaguzi huo.Moja ya matukio hayo,ni  jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa pasipo sababu ya msingi kwa kuwakamata wananchi na viongozi wa upinzani.Kwa mfano kuna baadhi ya wananchi  na viongozi wa upinzani kama Dk Kiiza Besigye kukamatwa na jeshi la polisi zaidi ya mara mbili na ofisi ya Chama Chake Cha FDC kuvamiwa pasipo sababu za msingi.Tatu ni nyumba za viongozi wa upinzani kama Amama Mbabazi kuzingirwa na jeshi la polisi nyakati tofauti
Hayo ni matukio makubwa yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha uchaguzi.Hata hivyo, kuna kasoro mbalimbali zilizojitokeza kipindi hicho,na kasoro hizo ni vituo vya kupigia kura kufunguliwa mapema lakini vifaa vya kupigia kura kutokifa vituoni mapema na kuletwa dakika za mwisho muda wa kupiga kura ukiwa unakaribia kuisha na matokeo ya uchaguzi vituoni kuzidi idadi halisi ya wananchi waliojiandikisha katika vituo hivyo.Kwa hiyo matukio hayo na kasoro hizo zinabaki kuibua maswali mengi kwa watu wengi.
Maswali hayo yanayoibuka ndani ya vichwa vya watu wengi ni kwanini  jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa  kukamata wananchi na viongozi wa upinzani na kuvamia ofisi za vyama vyao  pasipo sababu za msingi na walifanya hivyo kwa malengo yapi na kutumwa na nani?. Na inakuaje kasoro nyingi, mfano namba ya wapiga kura kuzidi namba halisi ya watu waliojiandikisha katika vituo hivyo?Je chombo husika yaani tume hawakuwa wamejiandaa kukabiliana na aina ya udanganyifu wowote, au tume iliamua kufumbia macho kasoro hizo kwa kuweza kukibeba chama kilichokuwa madarakani?
Kama Afrika tumeamua kukubali mfumo wa vyama vingi basi tuwe tayari kukabiliana na matokeo ya mfumo huo,ni dhahiri na imezoeleka kuwa vyama vinavyokuwa madarakani  pale uchaguzi unapokaribia kufanyika matukio mengi yamekuwa yakijitokeza,yaani serikali iliyopo madarakani kutumia kila njia kutaka kushinda uchaguzi kwa kukiuka taratibu na kujenga taswira machoni  mwa watu kwa  vyama vya upinzani  kuonekana kama  chanzo cha vurugu katika chaguzi.
Nafikiri  ifike pahala watawala watambue kuwa vyama vya upinzani vinaweza kuongoza nchi kama wananchi wameamua kuvipa ridhaa,hivyo maamuzi hayo yaheshimiwe kwa sababu wananchi ndiyo wenye nchi na ni jukumu lao kuamua nani atakuwa kiongozi wao, isitumike nguvu kubwa ya chama tawala kutumia nguvu dora kuhakikisha uamzi wa watu unaingiliwa.Tumeamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi,hivyo tuwe tayari kukubali matokeo ya mfumo huo.
Chagulani,Shabiru

25.2.2016

2/10/2016

Mazungumzo ni bora kuliko uchaguzi kurudiwa Zanzibar

Mwaka 2015 ulikuwa mwaka wa kihistoria katika jamhuri ya muungano wa Tanzania, yaani kwa kuwa na matukio makubwa, tukio la kwanza ni uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25,2015.Nauhita mwaka wa kihistoria kutokana na kampeni za uchaguzi pamoja na uchaguzi wenye kuwa na tofauti na miaka mingine iliyopita toka nchi ipate uhuru.Utofauti huo ni ushindani mkubwa uliokuwepo kwa vyama vya siasa na jinsi kampeni zilivyoendeshwa.Uchaguzi kwa Tanzania bara naweza kusema ulifanyika vizuri pamoja na kasoro za hapa na pale kujitokeza lakini kwa Tanzania visiwani yaani Zanzibar zoezi la uchaguzi halikumalizika vizuri kwa  maana ya matokeo ya uchaguzi kufutwa.
Uchaguzi huo ulifutwa kwa kile kinachodaiwa kuwa uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi ambazo zilipelekea chombo chenye mamalaka yaani tume ya uchaguzi Zanzibar( ZEC) kupitia mwenyekiti wake kutangaza kufutwa kwa uchaguzi kwa sababu kuu niliyoileza hapo awali.Hali hiyo imepelekea kile kinachoitwa mkwamo wa kisiasa( Political impasse).Mkwamo huo wa kisiasa umeibua maswali mengi kwa watu mbalimbali na taasisi mbali mbali,kwa mujibu wa waangalizi wa ndani na nje wanasema zoezi lilienda vizuri hakuna kasoro zilizojitokeza kama inavyodaiwa na tume,wapo wengine wanauliza uhalali wa tume kwa maana ya tume kuwa zinajitokezaje kasoro kubwa zinazopelekea mpaka matokeo yote ya ya uchaguzi kufutwa, je tume haikuwa imejiandaa kuhakikisha zoezi linafanyika kwa weredi? Na wengine wanadai kitendo cha mwenyekiti kufuta matokeo bila kamati kukaa ni kinyume cha sheria kwa mujibu wa sheria ilivyo/inavoelekeza.
Hatuwezi kupuuza wasiwasi wa watu hao walionao juu ya kilichotokea Zanzibar.Kama  wakaguzi wa ndani na nje walijiridhisha na kuweza kutoa taarifa juu ya zoezi la uchaguzi kwenda vizuri,kwa nini tume ya uchaguzi iliamua kufuta matokeo ya uchaguzi huo?, je tume imeamua kufanya hivyo kwa maslahi ya nani?,mimi siamini kama matokeo yote yanaweza kuwa na kasoro wakati kuna watu maalum walikuwepo wakisimamia zoezi hilo kuhakikisha linafanyika vizuri. Kama tume imeamua kuchukua uamzi huo kwa maslahi ya watu wachache au chama,itambue kufanya hivyo ni kinyume na demokrasia na nikinyume na katiba,kama tuliamua kuwa nchi ya kidemokrasia na kuruhusu mfumo wa vyama vingi basi hatuna budi kukubaliana na matokeo ya mfumo huo.
Afrika imekuwa na changamoto kubwa hasa linapokuja suala la demokrasia na mfumo wa vyama vingi,vyama tawala vimekuwa vikitumia nguvu dora  kufunja sheria  na kukiuka katiba hasa vinapoonekana kuelekea kushindwa na vyama vya upinzani katika chaguzi,nafikiri hili ndilo limekuwa likipelekea hata matokeo ya uchaguzi kufutwa au kuchelewa kutangazwa kwa baadhi ya vituo vya uchaguzi.Nadhani  vyama tawala vinasahau kuwa wananchi ndiyo wenye nchi,hivyo wakiamua kuchagua chama wanachokiona kwao ni sahihi  hakuna sababu ya kutumia nguvu dora na ukiukwaji wa katiba kwa kupindisha sheria na kumweka mtu ambaye chama tawala kinamtaka,wananchi wameamua hivyo lazima tuheshimu maamuzi yao.Kama wazanzibari wameamua kumchagua wanayemtaka basi tuheshimu maamuzi yao na hiyo ndiyo demokrasia ya kweli.
Baada ya matokeo ya uchaguzi kufutwa ,tume hivi karibuni ilitangaza tarehe ya uchaguzi kurudiwa yaani tarehe 20 Machi,2016.Sikuona sababu ya msingi ya uchaguzi kurudiwa,huu mkwamo wa kisiasa ungeweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya pande mbili kufanyika yaani CCM na CUF.Nikinukuu maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi hivi majuzi katika sherehe za maadhimisho ya Chama cha Mapinduzi kutimiza miaka 39,”Alisema hakupenda uchaguzi urudiwe”.Nafikiri hiyo ingekuwa fursa  ya pande mbili yaaani CCM na CUF  kutanguliza maslahi ya taifa na mazungumzo kufanyika na hatimaye kufikia muafaka na matokeo kutangazwa.Kurudia  uchaguzi kwanza ni gharama na inaweza kupelekea wazanzibari kutokwa na imani na tume ya uchaguzi na mwisho inaweza kuleta uadui kwa vyama na serikali hasa kwa wananchi kuichukia serikali iliyopo na kuona hakuna sababu ya wao kushiriki katika chaguzi mbalimbali kwa sababu tume haiaminiki tena.
Mimi naamini, endapo Chama Cha Mapinduzi kikiamua kutanguliza maslahi ya taifa mbele basi  suluhu inaweza  kupatikana kwa urahisi,naamini mpaka sasa Chama Cha wananchi CUF kimeonesha ukomavu kwa kutaka suluhu iwepo.Hivyo fursa hiyo itumike vizuri kwa maslahi ya Zanzibar na Jamhuri ya muungano kwa ujumla .
Chagulani,Shabiru
10/2/2016