Je,
Magufuli atatukomboa?
Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi kilikua na vikao
ambavyo vilipelekea kumpitisha John Pombe Magufuli kama Mgombea Urais kupitia
CCM katika uchaguzi unaotegemewa
kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Kwanza, nachukua fursa hii kumpongeza kwa kupitishwa
na kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi utakao fanyika mwezi Oktoba,haikuwa
kazi rahisi kufikia uamzi huo lakini
kupitia vikao vilivyofanyika kwa muda mrefu hatimaye aliweza kupitishwa.
Leo katika makala haya tunaangalia kama mgombea huyo
anaweza kuwa Mwarobaini kwa matatizo ya wananchi na taifa kwa ujumla.
John Pombe Magufuli
ni mwanasiasa mwenye uzoefu mkubwa, hasa ukizingatia kuwa amekuwa waziri
kuanzia awamu ya tatu mpaka awamu ya nne, pia anasikifa kwa kuwa mchapakazi na
mtu mwenye maamuzi ya haraka katika
kutafuta ufumbuzi wa jambo lolote.Yote hayo yamedhihirika katika wizara
mbalimbali alizozipitia, hivyo ana uzoefu wa masuala mbalimbali katika wizara
mbalimbali na utendaji kwa ujumla.
Kwa mtazamo huu nilioeleza hapo juu, ndugu Magufuli
anaonekana kama malaika au mkombozi machoni mwa watu wengi, mtazamo huo unaweza
kufanana na ule wa watu waliokuwa nao mwaka 2005 kipindi Jakaya
Kikwete alipopitishwa na kuanza kufanya kampeini sehemu mbalimbali za nchi, wengi
walionekana kummunga mkono wakitegemea kuwa ndiye mkombozi wao, hivyo
waliimunga mkono na kuweza kushinda uchaguzi kwa asilimia kubwa. Hivyo hali hiyo
inaweza kujirudia tena mwaka huu katika
uchaguzi.
Ukisoma ibara ya 8 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya mwaka 1977 inasema hivi katika vifungu a,b na c ( a)”.Wananchi
ndiyo msingi wa mamlaka yote na serikali itapata madaraka na mamalaka yake yote
kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa katiba hii” ( b)”.lengo kuu la serikali litakuwa
ni ustawi wa wananchi” ( c)Serikali itawajibika kwa wananchi. Kwa nukuu
ya vifungu hivyo hapo juu, tunaweza kupima kama serikali ya awamu ya nne
iliweza kutimiza wajibu wake kikatiba kwa kuhakikisha ustawi wa wananchi wake,
kwanza katika; afya, maji, elimu, umeme na miundombinu. Nafikiri wewe msomaji wa makali hii unaweza kujua hali halisi ilivyo katika sekta ya afya
ambapo ni rahisi kwenda hospitali ukaambiwa hakuna dawa wala vifaa tiba hali ambayo
imekuwa ikiipelekea vifo hasa kwa mama wajawazito
na watoto, pili sote tunafahamu kuwa maji bado ni tatizo mijini na vijijini, elimu
nayo inayotolewa sio bora na inafahamika
uwepo wa changamoto mablimbali kt sekta ya elimu. Changamoto hizo tumekumbana
nazo ktk awamu ya nne kwa kipindi cha miaka kumi chini ya utawala wa Chama Cha
Mapinduzi kilichotoa ahadi ya “Maisha Bora kwa kila Mtanzania.”
Naamini Magufuli haya yote anayajua vizuri maana
amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka ishirini, pia ni miongoni mwa wabunge walioshuhudia
matukio ya ufisadi toka awamu ya tatu
mpaka ya nne, lkn alishiriki katika bunge maalum la katiba na kuweza
kupitisha katiba pendekezwa ya CCM na
kupuuza ile iliyokuwa imependekezwa na wananchi.Je mnawezaje kumpa ridhaa mtu
huyu ambaye anaamini katika maslahi ya chama kwanza kuliko taifa?.
Nafikiri ifike pahala watanzania tuache ugonjwa wa kusahau tuliyoyapitia ktk
awamu ya nne.Tutakuwa tunajidanganya kutegemea
ukombozi wa kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya taifa kupitia Chama
Cha Mapinduzi, tumeshuhudia mengi
bungeni ambapo wabunge walionekana wapo tayari kutetea uovu kwa vijembe na kejeli kwa maslahi ya chama, pili
wamekuwa tayari kufanyanya lolote hata kama linakiuka sheria kanuni na
utaratibu ili kutimiza maslahi ya chama bila kujali lolote linazoweza
kujitokeza na kuathiri uchumi wa taifa,hii inaweza kudhihirishwa na utetezi wa
wabunge wa CCM ktk skendo ya escrow,pia tumeshuhudia miswada ya gesi na mafuta
ikipitishwa akidi bila kutia na wadau mbali mbali bila kushirikishwa na miswada
kutojadiliwa kwa kina.
Kwa kuhitimisha, Chama Cha Mapinduzi hakipo tayari
kumkoboa mwananchi na kuhakikisha ustawi wake na Taifa kwa ujumla.Miaka kumi inayoelekea ukomo wake
Oktoba inaweza kusaidia katika kufanya tathimini.Tuna mengi yakujifunza kwa
kufanya maamuzi kama wenzetu Kenya na Nigeria walivyofanya.
Kura yako ni silaha yako, itumie vizuri
Chagulani, Shabie
No comments:
Post a Comment