Je kodi inakusanywa ipasavyo ili
kuleta maendeleo?
Ni dhahiri
kua serikali yoyote duniani ili iweze kuendeshwa lazima ihakikishe wananchi
wanalipa kodi mbalimbali kuwezesha
shughuli za serikali kufanyika, ikiwemo kuhudumia wananchi wake katika
huduma mbalimbali mfano maji,afya,elimu na kadhalika .
Ni miezi
mitatu imepita kodi ya laini ya simu(sim
card tax) imepitishwa na serikali, na Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imeziandikia barua kampuni za simu kuzitaka kuanza kukata kodi hiyo kwa kila mtumiaji
mwenye laini ya simu,hivyo ( TRA ) imeagiza kukata kodi kuanzia mwezi wa saba
mpaka sasa kwa maana mwananchi hana budi kulipa shillingi elfu
tatu .Taifa lolote ili liendelee lazima likusanye kodi kama vyanzo vya mapato
katika kuendesha shughuli mbalimbali za serikali hivyo kila mwananchi hana
wajibu wa kulipa kodi kwa maana ya kuwa mfanyakazi ,mfanyabiashara kutokana na
biashara au kazi afanyayo na kodi nyingine ukusanywa na kulipwa kupitia
manunuzi ya bidhaa mbalimbali .
Mapato yanayokusanywa na serikali kupitia kodi mbalimbali serikali haina budi kuyarudisha kwa
wananchi kwa kuhakikissha wananchi wanapata huduma bora katika elimu,maji , afya
na huduma nyingine. Mfano kupitia kodi inayokusanywa na serikali tunategemea
katika vituo vya afya madawa na
vifaa tiba viwepo ili kuwezesha wananchi kupata matibabu kwa urahisi lakini kwetu hapa huduma zimeendelea kuwa
duni kila kukicha hasa maeneo ya vijijini
kutokana na mamlaka husika kutotekeleza
wajibu wake katika ukusanyaji wa kodi kama vyanzo vya mapato kwa serikali.
Hali hii ya kutokuwepo dhana ya uwajibikaji
katika mamlaka husika zilizopewa dhamana ya kuhakikisha kodi inalipwa
inapelekea wafanyabiashara wakubwa na hata makapuni makubwa kutokulipa kodi ipasavyo na hata yakilipa kodi ni kwa kiasi
kidodo ukilinganisha ukubwa na uzalishaji wa makampuni hayo, na wafanya
biashara wadogowadogo wamekua wakilipa kodi lakini hawatengezewi miundo mbinu
itakayowawezesha biashara yao kua
endelevu na hatimae hunyanyaswa kwa kufungiwa
biashara zao na wakati mwingine uendesha shughuli zao katika mazingira yasiyo
rafiki
Wakati mwingine umekuwepo misamaha ya
kodi kwa makampuni tajiri ya madini wakati makampuni haya yamekua
yakipata faida kubwa sana kupita kiasi na kukataa kueleza wazi mapato
wanayoyapata mfano makapumpuni ya simu
yamekua hayalipi kodi inayotakiwa ukilinganisha na faida inayopatikana kupitia
mitandao hiyo ya simu.
Hali hii inatokana na mamlaka husika
kutotokeleza wajibu wake ipasavyo na
kutokuwepo kwa uadilifu katika ukusanyaji wa mapato hasa kwa makampuni makubwa
kama ya simu na migodi pale maafisa wa mamlaka hizo wanapotengewa kiasi kikubwa
cha fedha na makampuni hayo na hatimae kiasi kidogo ukusanywa na mwisho wa siku
mzigo uelekezwa kwa mwanachi wa kawaida( mlalahoi) asiyekua na uhakika wa kupata hata milo miwili kwa siku,mwananchi huyu atake
asitake lazima alipie kadi ya simu yake kwa kila mwezi kama serikali
ilivyoelekeza kupitia mamlaka ya mapato Tanzania.inasikitisha sana kuona
wafanyabiashara wakubwa wenye kumiliki makampuni makubwa pia wanakwepa kulipa kodi kutokana na
ushawishishi wa kifedha walio nao .
Serikali za
mataifa yaliyoendelea duniani yamejidhatiti zaidi katika ukusaji wa kodi
kwa uadilifu na uzalendo ili kuweza kupata mapato yatakayowezesha serikali
kuboresha huduma za jamii kwa wananchi wake lakini kwetu hapa wajanja wachache
wamejidhatiti katika kukwepa kodi na kuruhusu mianya ya rushwa ili zoezi la ukusanyaji wa kodi kutofanyika kama inavyotakiwa na hali hii
huzolotesha kasi ya maendeleo kwa taifa
pale serikali inapojikuta ikikopa
pesa nje kwa ajili ya bajeti.
Chagulani Shabiru
Mwanza,Tanzania
2014
No comments:
Post a Comment