3/18/2015

Je,serikali inawajibika?



                                                   Je,  serikali inawajibika?
Serikali katika misingi ya kidemokrasia  ujipatia viongozi  wake kupitia uchaguzi unaofanyika sehemu husika.Viongozi hao wanaochagulia ndio baadae utengeneza serikali katika ngazi mbalimbali ili kuweza kutimiza majukumu ya kiserikali.Viongozi hawa ndiyo wanaokua wawakilishi wa wananchi katika shughuli mbalimbali za kiserikali, pia Kiongozi kama rais naye ufanya uteuzi  wa watu mbalimbali ili waweze kumsaidia katika idara mbalimbali kiutendaji ili kuweza  kufikia malengo kwa maendeleo na ustawi wa nchi husika.
      Hivyo serikali yenye kujua na kutambua wajibu wake ujikita zaidi kwa kuwajibika  ili kuweza kuhudumia wananch kwa kutumia rasilimali ilizonazo na kuwahakikishia ustawi uliokua mzuri kimaisha.Hivyo wananchi ujenga imani na serikali yao kwa  kuona serikali ikiwahakikishia ustawi wao katika Nyanja mbalimbali kama za kijamii na kiuchumi.
       Na serilikali zilizokua makini na zenye malengo ya dhati hutekeleza majukumu yao kwa kuhakiki wananchi mfano wafanya biashara wanapata mazingira mazuri yakuwezewsha biashara hizo kufanyika kwa urahisi na mazingira rafiki, hivyo watu hawa uweza kujipatia kipato kupitia biashara zao na kuweza kuendesha familia zao na pia serikali ukusanya kodi kwa wafanya biashara hawa.
    Kodi inayopatikana kama mapato hutumiwa na serikali katika kuendesha shughuli zake kwa kutoa huduma kwa wanachi  mfano  kama upatikanaji wa vifaa tiba na mdawa hospitalini ili kuweza kuhudumia wagonjwa kwa kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi.vilevile  wananchi watataraji kupata huduma za maji ili kuweza kurahisisha shughuli zao na pia watatarajia serikali inahakikisha uwepo wa elimu bora kwa uwepo wa watalam, mazingira bora yakufundishia na vifaa bora vya kufundishia .
          Upatikanji wa huduma hizo muhimu kwa wananchi utekelezwa na serilali yenye ni ya dhati kuona taifa linapiga hatua kimaendeleo katika nyanja mbalimbali .lakini kwetu hapa mambo yamekua tofauti na jinsi wananchi walivyotaraji kua uwepo wa serikali madarakani kuwa ni heri kwa mfano baada ya uchaguzi kufanyika serikali uonekana kama vile inasahau wajibu wake mfano katika elimu mazingira ya kufundishia saio rafiki, vifaa vya kufundishia hakuna  hali hii upelekea utendaji kazi katika sehumu hiyo kuwa mgumu na hatimaye ufaulu ushuka na elimu pia ushuka hili lipo wazi kwa matokeo ya kidato cha nnea yaliyopita yalikua mabaya na hatujaona hatua zilizochukuliwa ili kutatua tatizo hili.
        Katika afya pia huduma bado ni duni hasa katika upatikanaji kwa maana ya vituo kuwa  mbali hasa maeneo ya vijijini ambapo wananchi ulazimika kutembea umbali mrefu kili kuweza kupata huduma  .Na hata wakifika vifaa tiba hakuna hivyo hali hii upelekea vifo hasa kwa mama wajawazito wanaotembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo huko vijijni,na mijini vuilevile huduma ni duni  madawa na watalaam hakuna hii nayo uwafanya wataalam kutofika vituo vya kazi maana mazingira sio rafiki na hatimaye kimbilio lao ni nje ya nchi. Mfano Botswana ndio limekua kimbilio la madaktali wengi kutoka Tanzania.
    Upatikanaji wa maji nalo ni kero kwa wanachi mijini na vijijini pia. Vijijini watu usafiri umbali mrefu  wakati wa usiku hasa akina mama ili kuweza kupata maji kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za nyumbani.MIjini pia maji nayo ni ya mgao na sehemu nyingine hayapatikani kabisa wananchi ulazimika  wakati mwingine kununua maji kwa gharama kubwa,kutopatikana kwa maji upelekea kukwama kwa shughuli za uzalishaji hata za nyumabani pia,tatizo hili lipo maeneo mengi hasa Dar es  salaam,Morogoro,Singida na Dodoma.
       Umasikini nao umezidi kuongezeka kwa wananchi kila kukicha.Hi inatokana na serikali kutotumia rasilimali ilizonazo ili kuwatengeneza wananchi fursa ili nao waweze kujiinua kimaisha, na badala ake serikali kuwanyanyasa wananchi pale wanapojishughulisha kwa kuanzisha  biasharara ndogondogo kwa kuwatoza kodi bila kuwaboreshea mazingira salama kwa ajili ya kuendesha shughuli zao na wakati mwingine wajasiriamali hao ufukuzwa na serikali bila hata kutafutiwa sehemu nyingine ya kuweza kueendeshea buiashara zao. Hali upelekea watu kutokua na uhakika hata wa kupata kipato  cha kuweza kumudu maisha yao
       Ni jukumu la serikali kuakikisha wananchi na mali zao wanakua salama kupitia mamlaka zake.Kwetu hapa usalama wa raia uko mashakani  hii ipo wazi na linadhihirishwa na matukio mengi ambayo yamekua yakitokea hapa nchini watu kupotza uhai na hata mali zao pia, mfano hivi majuzi tumempoteza Dr Sengondo Mvungi aliyevamiwa nyumbani kwake huko kibamba. Pia  malalamiko mengi yamekua yakitolewa juu ya utendaji wa jeshi la polisi kukamata watu ovyo na pengine mtu kutosikilizwa na hatimae jeshi la polisi ufikia uamzi wa kufanyanya lolote lile kwa jinsi litakavyo dhidi ya raia.
     Serikali makini kote duniani ukemea vikali masuala ya rushwa. Hapa kwetu ni tofauti kidogo kwa maana ya mamlaka husika uonekana kua wakali kwa matukio madogo madogo ya rushwa lakini mamlaka hizi ushindwa kutekeleza wajibu wake pale tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi wa umma zinapotokea na hatua uchukua muda mrefu kuchukuliwa kwa kisingizio cha uchunguzi  unafanyika . Mfano tuhuma mbalimbali zimekua kikitolewa juu ya baadhi ya viongozi wa serikali  lakini hakuna chochote kinachofanyika .Hali hii upelekea kushamiri kwa vitendo hivyo kama ilivyo sasa.
Serikali makini inapopata ridhaa ya kuwa madarakani, jukumu lake kubwa ni kuhakikisha  ustawi wa wananchi wake unakua bora  ili kuweza kupiga hatua kimaendeleo katika nyanja zote na sio kufikiria uchaguzi mwingine pale wanapo pewa na ridhaa na wananchi.
   Chagulani Shabiru
   Mwanza, Tanzania
2014

No comments:

Post a Comment