Tusitarajie katiba mpya kwa sasa
Katiba ni
mwongozo wenye sheria na kanuni mbalimbali kwa ajili ya uendeshaji wa
nchi.Mataifa yaliyo makini duniani uruhusu
utaratibu uliokuwa bora kwa kuwashirikisha wananchi katika upatikanaji
wa katiba kwa kukusanya maoni yao na kuyafanyia uchambuzi kupitia tume na kisha
katiba kutungwa kwa kuzingatia maoni yaliyopendekezawa na wananchi.
Katika mchakato wa kutafuta katiba mpya mh rais
aliteua tume iliyokusanya maoni na kuyafanyia uchambuzi wa kina na badae
likawepo bunge maalum la katiba ambalo lilijumuisha wajumbe mbali mbali kama wabunge wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania ambao walipatikana kwa sheria iliyopitishwa na bunge nao kuwa sehemu
ya bunge maalum la katiba, na wajumbe wengine ni kutoka vyama vya siasa,asasi
zisizo za kiraia ambao waliteuliwa na
Rais.
Baada ya uteuzi wa wajumbe wa bunge maalum la katiba
,kazi yao kubwa ilikua ni kusimamia
rasimu kwa kujadili maoni yaliyotolewa na wananchi na kuyaboresha pia. Suala la kusimamia maoni ya wananchi
kwenye rasimu linaonekana kutozingatiwa, hili linadhihirishwa kwa baadhi ya vifungu vilivyoko kwenye rasimu
kuodolewa ,mfano ni kifungu kilichokuwa kikizungumzia tunu za taifa ambazo ni
uadilifu,uzalendo na uwajibikaji.Kifungu hiki kimepuuzwa na wajumbe kutoka
chama tawala, na hali hiyo ilipelekea umoja wa katiba ya wananchi ( UKAWA) na baadhi ya
wajumbe wengine kutoka bungeni kwa kutoridhiswa na mwenendo wa bunge .
Na kuanza kwa awamu ya pili kwa bunge maalum la
katiba kumetiliwa shaka hasa ukizingatia baadhi ya wajumbe waliotoka nje hapo
awali, kwa kutoridhishwa na jinsi bunge lilivyokuwa likifanya kazi na jitihada
za kuhakikisha wajumbe hao kurejea bungeni zikigonga mwamba kutokana na
kutofikiwa kwa maridhiano kwa pande zote
mbili,Hali hii imepelekea upande mmoja yaani wajumbe ambao ni sehemu kubwa ya
Chama cha Mapinduzi wao kuonekana ndiyo wenye dhamana ya kuhakikisha katiba
inapatikana.
Uwepo huu wa idadi kubwa ya wajumbe ambao ni sehumu
ya chama tawala kuendelea na bunge maalum unatiliwa shaka,hii nikutokana
wajumbe hao kuondoa kifungu cha wananchi kuwajibisha mbunge na ukomo wa
ubunge,kitendo hiki kinaashiria wajumbe kulinda maslahi binafsi kwa kushindwa
kusimamia maoni ya wananchi kwa kuyaboresha na badala yake wanaondoa vifungu
ambavyo vinaonekana kwao vinaweza kuwa havina maslahi,kufanya hivi ni kinyume
na jukumu la bunge maalum la katiba.
Kwa hatua hii bunge kutawaliwa na hisia na kushindwa
kujikita katika kujadili maoni ya wananchi ni kiashiria tosha kuwa uwezekano wa
kupata katiba bora iliyotokana na maoni
ya wananchi ni mdogo,hii ni kutokana na hali halisi inayoendelea kwa baadhi ya
wajumbe kuwa nje ya bunge na mjadala ukiendelea bungeni na waliobaki bungeni
kutotimiza majukumu yao na badala yake mchakato kutekwa na msimamo wa chama na
wakati mwingine hali hii kuonekana kama fursa kwa baadhi ya wajumbe kama
washindi ( winners) kwa kuendelea kubaki bungeni na walioondoka kuonekana
kama walioshindwa ( losers)
Na historia inaonyesha udhaifu wa bunge letu kutumia wingi wao
kufanya maamuzi hata kama hayana tija kwa wananchi ilimradi yana maslahi kwa
chama kinachounda serikali, hivyo hii dhana ya winners na losers inaweza
kupelekea maamuzi kufanyika vibaya
ilimradi yaa tija kwa watawala,nadhani ungekuwa wakati mzuri sasa kwa
kujifunza kutoka kwa majirani zetu kama
Kenya walioweka tofauti zao pembeni na kutanguliza maslahi ya taifa mbele
katika upatikanaji wa katiba.
Mwisho kabisa,upatikanaji wa katiba ni maridhiano
kwa kuweka misimamo ya vyama pembeni na kusimamia rasimu iliyotokana na maoni
yalitolewa na wananchi na itakayodumu kwa miaka mingi ijayo .kutopatikana kwa
katiba itakuwa ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi zilizotumika kuendesha
bunge na kulipa posho wajumbe, na
wananchi watakuwa hawajatendewa haki kwa pesa zao kutumika vibaya .
Chagulani Shabiru
Kutoka St. Augustine, Mwanza.
2014
No comments:
Post a Comment